Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Hujjatul Islam wal Muslimin Sayyid Mahdi Khamoushi, Mkuu wa Taasisi ya Awqaf na Masuala ya Kheri, katika hafla ya kuwakabidhi rasmi viongozi wa Kamati ya Maandalizi ya Mashindano ya 48 ya Kitaifa ya Qur’an Tukufu, alisisitiza nafasi ya Qur’an katika kuongoza jamii ya Kiislamu na kusema: “Katika miaka ya hivi karibuni, tumekuwa tukizungumza kuhusu kigezo cha ukamilifu na kusimama kidete. Neno muqawama (kusimama imara/ Muqawamah) limetajwa mara nyingi katika Qur’an, lakini kiini cha yote hayo ni kauli ya Qur’an: "Ihdinas-Siratal-Mustaqim" (Tuongoze njia iliyo nyooka).”
Akaongeza: “Kama Qur’an haingekuwa ndio inayotuonesha na kutuongoza njia, basi kunyenyekea mbele ya mabeberu kungekuwa halali, lakini leo hii kusimama imara (Muqawamah/ Upinzani) dhidi yao ni fahari ya Waumini.Msimamo wa kimantiki wa Kiongozi mpendwa wa Mapinduzi umekuwa gumzo ulimwenguni.”
Khamoushi aligusia jinai za karibuni za utawala wa Kizayuni huko Gaza na kusema: “Hebu angalia maovu ambayo maadui wamewatendea watu wa Gaza; karibu watu milioni tatu wamepoteza makaazi yao. Tulijibu uvamizi wao dhidi ya nchi yetu, na iwapo watajaribu tena kufanya kosa hilo, jibu letu safari hii litakuwa kali zaidi.”
Aidha, alitaja ahadi za Mwenyezi Mungu kwa kusema: “Mwenyezi Mungu haumuachii dunia watu wachafu. Huupamba upande wa haki na kuupiga upande wa batili. Mwenyezi Mungu ni mkweli katika ahadi zake, na iwapo imani itaingia ndani ya nyoyo, basi hakuna la kuogopa. Imani ya kumtegemea Mmoja tu wa kweli ni kuamini kwamba Allah hatotuacha peke yetu.”
Akizungumzia jukumu la Taasisi ya Awqaf katika kueneza mtindo wa maisha wa Kiqur’an, Khamoushi alisema: “Kazi yetu kuu ni kuinua bendera ya Qur’an ili kwa kueneza mtindo sahihi wa maisha, jamii ya Kiqur’ani iweze kuundwa. Ikiwa nchi za Kiislamu zitaifuata Qur’an, zitauweza kuwalazimisha maadui kurudi nyuma.”
Your Comment